Biblia inasema nini kuhusu Hekima – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hekima

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hekima

Mwanzo 41 : 16
16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.

Mwanzo 41 : 39
39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.

Matendo 7 : 10
10 ⑧ akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.

Matendo 7 : 22
22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.

Kutoka 31 : 5
5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Kutoka 35 : 35
35 ⑪ Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

Kutoka 36 : 1
1 ⑫ Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.

Kutoka 31 : 6
6 ② Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza;

Kutoka 35 : 35
35 ⑪ Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

Kutoka 36 : 1
1 ⑫ Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.

Kutoka 36 : 2
2 ⑬ Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;

Kutoka 35 : 26
26 Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi.

1 Wafalme 7 : 14
14 ⑤ Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.

2 Mambo ya Nyakati 2 : 14
14 mwana wa mwanamke wa kabila la Dani, na babaye alikuwa mkazi wa Tiro, yeye ni bingwa wa kutumia dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mti; na wa nguo za urujuani, samawati, nyekundu na kitani safi; tena ni stadi kwa kutia nakshi na kuchora michoro yoyote, mbunifu na kuchora chochote kufuatana na kielekezo ambacho angepewa yeye na watu wako mastadi wa bwana wangu Daudi baba yako.

1 Wafalme 3 : 12
12 ② basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

1 Wafalme 3 : 28
28 ⑧ Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.

1 Wafalme 4 : 34
34 Watu wakaja kutoka mataifa yote, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake, ili waisikie hekima ya Sulemani.

1 Wafalme 5 : 12
12 BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanya mikataba kati yao wawili.

1 Wafalme 10 : 24
24 Ulimwengu wote ukamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.

1 Wafalme 4 : 31
31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.

1 Mambo ya Nyakati 12 : 32
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *