Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ham
Mwanzo 5 : 32
32 Baada ya Nuhu kufikisha umri wa miaka mia tano, aliwazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Mwanzo 9 : 18
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
Mwanzo 9 : 24
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 4
4 na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Mwanzo 9 : 27
27 ⑥ Mungu amwongezee Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.
Mwanzo 10 : 20
20 Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 16
16 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 40
40 Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
Zaburi 78 : 51
51 ⑥ Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.
Zaburi 105 : 23
23 ⑥ Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.
Zaburi 105 : 27
27 Akatenda mambo ya ishara zake kati yao, Na miujiza katika nchi ya Hamu.
Zaburi 106 : 22
22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye Bahari ya Shamu.
Mwanzo 14 : 5
5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
Leave a Reply