Biblia inasema nini kuhusu Hakimu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hakimu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hakimu

Ezra 7 : 25
25 ⑲ Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke mahakimu na majaji, watakaowaamua watu wote walio ng’ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; na ukamfundishe yeye asiyezijua.

2 Samweli 8 : 15
15 Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.

2 Samweli 15 : 2
2 ⑤ Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu yeyote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumishi wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli.

1 Wafalme 3 : 28
28 ⑧ Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.

1 Wafalme 10 : 9
9 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti cha enzi cha Israeli; kwa kuwa BWANA amewapenda Israeli milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme, ufanye hukumu na haki.

2 Wafalme 8 : 6
6 Na mfalme alipomwuliza yule mwanamke, yeye akamweleza. Basi mfalme akamtolea ofisa, akasema, Mrudishie yote aliyokuwa nayo, na mapato yote ya shamba lake tangu siku aliposafiri, hata leo.

Zaburi 72 : 4
4 Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.

Mathayo 27 : 26
26 Ndipo akawafungulia Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa ili asulubiwe.

Matendo 23 : 35
35 akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.

Matendo 25 : 12
12 Basi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufani kwa Kaisari! Basi, utakwenda kwa Kaisari.

Kumbukumbu la Torati 17 : 9
9 uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonesha hukumu ya maamuzi;

2 Mambo ya Nyakati 19 : 8
8 Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi kwa hukumu za BWANA na kesi kati yao. Nao wakarudi Yerusalemu.

Ezekieli 44 : 24
24 Na katika mabishano watasimama ili kuamua; wataamua kulingana na hukumu zangu; nao watazishika sheria zangu, na amri zangu, katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa; nao watazitakasa sabato zangu.

Mathayo 26 : 62
62 Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?

Waamuzi 4 : 4
4 Basi Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.

Kutoka 18 : 22
22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.

Kutoka 22 : 9
9 ⑮ Kila jambo la kukosana, kama ni la ng’ombe, au la punda, au la kondoo, au la mavazi, au la kitu chochote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele ya Mungu; na yeye atakayehukumiwa na Mungu kuwa ni mkosa atamlipa mwenziwe thamani yake mara mbili.

Kutoka 22 : 28
28 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *