Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Haki
Kutoka 23 : 3
3 wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.
Kutoka 23 : 8
8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.
Mambo ya Walawi 19 : 15
15 ⑲ Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Kumbukumbu la Torati 16 : 20
20 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 25 : 4
4 ⑲ Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.
Ezra 7 : 26
26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kali, iwe ni kuuawa, au ni kuhamishwa, au kunyang’anywa mali yake, au kufungwa.
Zaburi 72 : 2
2 ⑯ Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
Zaburi 82 : 4
4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
Mithali 17 : 15
15 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Mithali 17 : 26
26 Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si vyema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.
Mithali 18 : 5
5 Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
Mithali 18 : 17
17 Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza.
Mithali 20 : 8
8 Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.
Mithali 22 : 27
27 Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?
Mithali 24 : 23
23 ④ Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema.
Mithali 28 : 21
21 ④ Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.
Mithali 29 : 26
26 Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA
Mhubiri 3 : 17
17 ⑱ Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.
Mhubiri 5 : 8
8 Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.
Mhubiri 7 : 7
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
Isaya 1 : 17
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Isaya 56 : 1
1 BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.
Isaya 59 : 15
15 Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki.
Yeremia 22 : 4
4 ⑯ Kwa maana mkifanya haya kweli kweli, ndipo watakapoingia kwa malango ya nyumba hii wafalme wenye kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi, wanakwenda kwa magari, na wamepanda farasi, yeye, na watumishi wake, na watu wake.
Maombolezo 3 : 36
36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa.
Amosi 5 : 7
7 Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,
Amosi 5 : 12
12 ⑰ Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.
Mika 7 : 3
3 Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Leave a Reply