Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hadadezeri
2 Samweli 8 : 13
13 ④ Basi Daudi akajipatia jina, alipokuwa akirudi, aliwaua Waedomi elfu kumi na nne katika bonde la chumvi.
2 Samweli 10 : 19
19 Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia Waamoni tena.
1 Wafalme 11 : 23
23 ⑮ Tena, Mungu akamwinulia adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba,
1 Mambo ya Nyakati 18 : 10
10 akamtuma mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote.
1 Mambo ya Nyakati 19 : 19
19 Na watumishi wa Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Daudi, wakamtumikia; wala Washami hawakukubali kuwasaidia wana wa Amoni tena.
Leave a Reply