Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gosheni
Mwanzo 45 : 10
10 ⑮ Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng’ombe wako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko;
Mwanzo 46 : 28
28 Yakobo akamtuma Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni.
Kutoka 8 : 22
22 Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao inzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.
Kutoka 9 : 26
26 Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe.
Yoshua 10 : 41
41 ④ Yoshua akawapiga kutoka Kadesh-barnea mpaka Gaza, na nchi yote ya Gosheni, hata Gibeoni.
Yoshua 11 : 16
16 ⑬ Hivyo Yoshua akatwaa nchi hiyo yote, hiyo nchi ya vilima, na nchi yote ya Negebu, na nchi yote ya Gosheni, na hiyo Shefela, na hiyo Araba na nchi ya vilima vilima ya Israeli, na hiyo nchi tambarare;
Yoshua 15 : 51
51 ⑤ Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.
Leave a Reply