Biblia inasema nini kuhusu giza – Mistari yote ya Biblia kuhusu giza

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia giza

Yohana 1 : 5
5 Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

1 Yohana 1 : 5 – 7
5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lolote hamna ndani yake.
6 Tukisema ya kwamba tunashirikiana naye, huku tukienenda katika giza, tunasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
7 bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Yohana 11 : 10
10 ⑩ Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.

Luka 1 : 79
79 ⑯ Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.

Matendo 26 : 18
18 ⑳ uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.

Zaburi 139 : 12
12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.

Yohana 3 : 19 – 21
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

1 Wathesalonike 5 : 5
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

2 Wakorintho 6 : 14
14 ⑭ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

Yohana 8 : 12
12 ⑬ Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

1 Yohana 2 : 8 – 11
8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.
9 Yeye asemaye kwamba yumo katika nuru, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

Wakolosai 1 : 13
13 Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa;

Ufunuo 9 : 2
2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuri kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

Waraka kwa Waebrania 12 : 18
18 Maana hamkufikia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,

Isaya 50 : 10
10 ⑥ Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.

Waefeso 5 : 8
8 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru,

Mathayo 8 : 12
12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 25 : 30
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

2 Petro 2 : 4
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;

Mwanzo 1 : 2
2 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *