Biblia inasema nini kuhusu Gamalieli – Mistari yote ya Biblia kuhusu Gamalieli

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Gamalieli

Matendo 5 : 40
40 Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Matendo 22 : 3
3 ⑧ Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; ⑩

Hesabu 1 : 10
10 Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.

Hesabu 2 : 20
20 Na karibu naye itakuwa kabila la Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri;

Hesabu 10 : 23
23 Tena juu ya jeshi la kabila la wana wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.

Hesabu 7 : 59
59 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *