Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Fox
Mathayo 8 : 20
20 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Luka 9 : 58
58 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.
Waamuzi 15 : 4
4 Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa mienge ya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia mwenge kati ya kila mikia miwili.
Zaburi 63 : 10
10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwamwitu.
Wimbo ulio Bora 2 : 15
15 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.
Nehemia 4 : 3
3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.
Ezekieli 13 : 4
4 Ee Israeli, manabii wako wamekuwa kama mbweha, mahali palipo ukiwa.
Luka 13 : 32
32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.
Wimbo ulio Bora 2 : 15
15 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.
Leave a Reply