Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Filakteria
Kutoka 13 : 9
9 Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo.
Kutoka 13 : 16
16 Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
Kumbukumbu la Torati 6 : 9
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
Kumbukumbu la Torati 11 : 18
18 Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
Mathayo 23 : 5
5 ⑧ Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Leave a Reply