Biblia inasema nini kuhusu falsafa – Mistari yote ya Biblia kuhusu falsafa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia falsafa

Wakolosai 2 : 8
8 ⑩ Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

Tito 3 : 9 – 10
9 ④ Lakini ujiepushe na mabishano ya kipumbavu, nasaba, magomvi, na mabishano ya sheria. Kwa kuwa hayana manufaa, tena hayafai kitu.
10 ⑤ Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, tengana naye;

1 Wakorintho 2 : 13
13 ⑦ Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

1 Timotheo 6 : 20
20 ③ Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;

1 Wakorintho 2 : 1 – 5
1 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubirie siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.
2 Maana niliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa.
3 Nami nilikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na kwa kutetemeka sana.
4 Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

1 Wakorintho 2 : 6 – 10
6 ① Lakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
7 ② bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 ③ ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu.
9 ④ Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
10 ⑤ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

1 Wakorintho 1 : 21
21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.

Wakolosai 2 : 16 – 19
16 ⑱ Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 ⑲ mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;
19 ⑳ wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.

Mhubiri 7 : 1 – 29
1 Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
5 Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
6 Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
8 ① Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
9 ② Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10 Usiseme, Kwa nini siku za kale zilikuwa ni bora kuliko siku hizi? Maana si kwa hekima unauliza hili.
11 Hekima ni njema kama urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionalo jua.
12 Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
13 ③ Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
15 ④ Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.
16 ⑤ Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwa nini kujiangamiza mwenyewe?
17 ⑥ Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
18 Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.
19 Hekima ni nguvu zake mwenye hekima, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.
20 ⑦ Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, atendaye mema pasipo kutenda dhambi.
21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote wasemayo watu; usije ukamsikia mtumishi wako mwenyewe akikutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine.
23 Mambo hayo yote mimi nimeyahakikisha katika hekima. Nilisema, Mimi nitakuwa na hekima, lakini imefarakana nami.
24 ⑧ Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana, ni mtu yupi awezaye kuyatafuta?
25 Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu.
26 Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
27 Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla;
28 ambayo bado nafsi yangu ningali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona.
29 ⑩ Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamepanga mipango mingi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *