Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia fahari
Yakobo 4 : 6
6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Mithali 16 : 18 – 19
18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Mithali 16 : 5
5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.
Waraka kwa Waebrania 11 : 6
6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Leave a Reply