Eliakimu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Eliakimu

Luka 3 : 30
30 wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,

2 Wafalme 18 : 18
18 Na walipokwisha kumwita mfalme, wakatokewa na Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe.

2 Wafalme 19 : 2
2 Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.

Isaya 36 : 3
3 Wakamtokea Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika kumbukumbu.

Isaya 36 : 11
11 Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule kamanda, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa watu wote walio ukutani.

Isaya 36 : 22
22 Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika kumbukumbu, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zikiwa zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule kamanda.

Isaya 37 : 2
2 Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wakiwa wamejivika nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi.

2 Wafalme 23 : 34
34 Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia awe mfalme mahali pa Yosia babaye, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu, lakini akamwondoa Yehoahazi; akaenda naye Misri, naye akafa huko.

2 Mambo ya Nyakati 36 : 4
4 Mfalme wa Misri akamtawaza Eliakimu nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, akambadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Neko akamtwaa Yehoahazi nduguye, akamchukua mpaka Misri.

Mathayo 1 : 13
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

1 Mambo ya Nyakati 3 : 21
21 Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.[1]

Nehemia 12 : 41
41 na makuhani, Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania, wenye baragumu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *