Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Efrata
Mwanzo 35 : 16
16 Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali.
Mwanzo 35 : 19
19 ⑲ Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.
Mwanzo 48 : 7
7 Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.
Ruthu 4 : 11
11 ⑰ Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Zaburi 132 : 6
6 ⑮ Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika shamba la Yearimu tuliiona.
Mika 5 : 2
2 ④ Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 19
19 Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrata, aliyemzalia Huri.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 50
50 Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;
1 Mambo ya Nyakati 4 : 4
4 na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu.
Leave a Reply