Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Dunia
Mwanzo 1 : 7
7 Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Ayubu 26 : 7
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
Zaburi 104 : 9
9 ⑳ Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
Isaya 45 : 18
18 Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.
1 Samweli 2 : 8
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
Ayubu 9 : 6
6 Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetemeka.
Ufunuo 7 : 1
1 ⑲ Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.
Mwanzo 3 : 18
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Warumi 8 : 22
22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina uchungu pamoja hata sasa.
Isaya 40 : 22
22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Isaya 66 : 1
1 BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
Maombolezo 2 : 1
1 Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.
Zaburi 115 : 16
16 Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.
Kumbukumbu la Torati 32 : 8
8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
Mwanzo 49 : 26
26 Baraka za baba yako Ni nyingi kuliko za milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake, yeye aliyeteuliwa kati ya ndugu zake.
Kumbukumbu la Torati 33 : 15
15 Na kwa vitu viteule vya milima ya kale, Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele,
Zaburi 78 : 69
69 ⑳ Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele.
Zaburi 104 : 5
5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele.
Mhubiri 1 : 4
4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
Habakuki 3 : 6
6 Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Isaya 65 : 17
17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.
Leave a Reply