Diboni

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Diboni

Hesabu 21 : 30
30 ⑪ Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni, Nasi tumeharibu mpaka Nofa, Ifikiayo Medeba.

Hesabu 33 : 45
45 ④ Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapiga kambi Dibon-gadi.

Hesabu 32 : 3
3 Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,

Hesabu 32 : 34
34 Kisha wana wa Gadi wakajenga Diboni, na Atarothi, na Aroeri;

Yoshua 13 : 9
9 kutoka huko Aroeri, iliyoko pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulioko pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni;

Yoshua 13 : 17
17 na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni;

Isaya 15 : 2
2 Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.

Isaya 15 : 9
9 Maana maji ya Dimoni yamejaa damu; maana ninatayarisha msiba mpya juu ya Dimoni, simba juu ya watu wa Moabu waliokimbia, na juu ya mabaki yao.

Yeremia 48 : 18
18 Ee binti ukaaye Diboni, Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu; Maana atekaye Moabu amepanda juu yako, Ameziharibu ngome zako.

Yeremia 48 : 22
22 na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;

Nehemia 11 : 25
25 ④ Na kuhusu habari za vijiji na mashamba yake; wengine wa wana wa Yuda walikuwa wakikaa Kiriath-arba na vijiji vyake, na katika Diboni na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake;

Yoshua 15 : 22
22 Kina, Dimona, Adada;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *