Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Cockatrice
Isaya 11 : 8
8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake katika pango la fira.
Isaya 14 : 29
29 Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7
Isaya 59 : 5
5 ③ Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
Yeremia 8 : 17
17 Maana, tazama, nitatuma nyoka, naam, fira, kati yenu, wasioweza kutumbuizwa kwa uganga; nao watawauma, asema BWANA.
Leave a Reply