Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Carmi
Mwanzo 46 : 9
9 Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.
Kutoka 6 : 14
14 Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 1
1 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 9
9 ⑧ Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 18
18 Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azuba, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.
Yoshua 7 : 1
1 ⑬ Lakini Waisraeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya Waisraeli.
Yoshua 7 : 18
18 Akawasongeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda akatwaliwa.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 7
7 ⑦ Na wana wa Karmi; Akani, yule aliyewataabisha Israeli, kwa kuchukua kilichowekwa wakfu.
Leave a Reply