Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Bibi arusi
Isaya 49 : 18
18 Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema BWANA, hakika utajivika hao wote kama pambo, nawe utajipamba kwao kama bibi arusi.
Isaya 61 : 10
10 Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Yeremia 2 : 32
32 ④ Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.
Ufunuo 21 : 2
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Mwanzo 24 : 53
53 ① Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
Mwanzo 24 : 59
59 ④ Ndipo wakampeleka Rebeka dada yao, na yaya wake, na mtumishi wa Abrahamu, na watu wake.
Mwanzo 24 : 61
61 Rebeka akaondoka na vijakazi wake, nao wakapanda juu ya ngamia, wakamfuata yule mtu. Naye huyo mtumishi akamchukua Rebeka akaenda zake.
Mwanzo 29 : 24
24 Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake.
Mwanzo 29 : 29
29 Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake.
Zaburi 45 : 17
17 ⑭ Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa watakushukuru Milele na milele.
Ezekieli 16 : 14
14 Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU.
Ufunuo 19 : 8
8 ⑱ Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing’aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
Ufunuo 21 : 2
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo 21 : 9
9 ⑦ Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana-kondoo.
Ufunuo 22 : 17
17 Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
Leave a Reply