Biblia inasema nini kuhusu Biashara – Mistari yote ya Biblia kuhusu Biashara

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Biashara

Mambo ya Walawi 19 : 37
37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.

Mambo ya Walawi 25 : 14
14 ⑩ Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;

Mambo ya Walawi 25 : 17
17 ⑪ Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Mwanzo 37 : 25
25 ⑧ Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.

Mwanzo 37 : 27
27 ⑪ Haya, na tumuuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali.

Isaya 60 : 6
6 ⑱ Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.

1 Wafalme 9 : 28
28 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta[20] mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.

1 Wafalme 10 : 11
11 Tena merikebu za Hiramu, zilizochukua dhahabu kutoka Ofiri, zikaleta kutoka Ofiri miti ya msandali mingi sana, na vito vya thamani.

1 Wafalme 22 : 48
48 Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; lakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi.

Zaburi 107 : 30
30 Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia Naye akawaleta mpaka bandani waliyoitamani.

Mithali 31 : 14
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.

Ufunuo 18 : 19
19 ③ Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

Ezekieli 27 : 12
12 Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa.

Ezekieli 27 : 19
19 Wedani, na Yavani, walifanya biashara toka Uzali kwa vitu vyako; chuma kilichofuliwa, na mdalasini, na mchai, vilikuwa katika bidhaa yako.

Mathayo 11 : 16
16 Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,

Isaya 60 : 6
6 ⑱ Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.

Yeremia 6 : 20
20 ① Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.

Ezekieli 27 : 24
24 Hao ndio waliokuwa wachuuzi wako, kwa vitu vya tunu, kwa vitumba vya nguo za samawati na kazi ya taraza, na masanduku ya mavazi ya thamani, yaliyofungwa kwa kamba, na kufanyizwa kwa mti wa mierezi, katika bidhaa yako.

Mwanzo 42 : 34
34 ⑯ Mkaniletee ndugu yenu mdogo; ndipo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi, bali ni watu wa kweli; basi nitawarudishia ndugu yenu, nanyi mtafanya biashara katika nchi hii.

Isaya 45 : 14
14 BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.

Mwanzo 37 : 28
28 ⑫ Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *