Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Basemathi
Mwanzo 26 : 34
34 ⑬ Esau alipokuwa mwenye miaka arubaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti.
Mwanzo 36 : 4
4 Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli.
Mwanzo 36 : 10
10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reueli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
Mwanzo 36 : 13
13 Na hawa ni wana wa Reueli: Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau.
Mwanzo 36 : 17
17 Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.
Leave a Reply