Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Barnaba
Matendo 13 : 1
1 ② Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri,[2] na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli.
Matendo 14 : 14
14 Lakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika umati wa watu, wakipiga kelele,
Matendo 4 : 37
37 alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.
Matendo 9 : 27
27 Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
Matendo 11 : 30
30 Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.
Matendo 12 : 25
25 ① Na Barnaba na Sauli, walipokwisha kutimiza huduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemu, wakamchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko.
Matendo 14 : 7
7 ① wakakaa huko, wakiihubiri Injili.
Matendo 14 : 18
18 Na kwa maneno hayo wakawazuia watu kwa shida, wasiwatolee dhabihu.
Matendo 14 : 20
20 Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na kesho yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba mpaka Derbe.
Wagalatia 2 : 9
9 tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
Matendo 15 : 39
39 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akaabiri kwenda Kipro.
Leave a Reply