Biblia inasema nini kuhusu baraka za nyumba – Mistari yote ya Biblia kuhusu baraka za nyumba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia baraka za nyumba

2 Samweli 7 : 28 – 29
28 Na sasa, Ee Bwana MUNGU, wewe ndiwe Mungu, na maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidia mtumishi wako jambo hili jema
29 basi, sasa, uwe radhi, ukaibariki nyumba ya mtumishi wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Ee Bwana MUNGU, umelinena na kwa baraka yako nyumba ya mtumishi wako na ibarikiwe milele.

Zaburi 122 : 7
7 Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.

Mathayo 7 : 24
24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

Hesabu 6 : 24
24 ⑪ BWANA akubariki, na kukulinda;

Zaburi 91 : 10 – 12
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

Zaburi 121 : 7 – 8
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Kumbukumbu la Torati 6 : 4 – 9
4 Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja[3]
5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Zaburi 127 : 1 – 5
1 BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
2 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3 Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.
4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.
5 Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.

Isaya 41 : 10
10 ② usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.

Kumbukumbu la Torati 28 : 3 – 8
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
7 BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.

Hagai 2 : 7 – 9
7 nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema BWANA wa majeshi.
8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi.
9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi.

Yoshua 24 : 15
15 ⑭ Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Zaburi 121 : 1 – 8
1 Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Mithali 24 : 3
3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *