Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Barabara
Kumbukumbu la Torati 2 : 27
27 Nipishe katikati ya nchi yako; nitakwenda kwa njia ya barabara, sitageuka kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto.
Yoshua 10 : 10
10 BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.
Waamuzi 21 : 19
19 Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, mji ulio upande wa kaskazini mwa Betheli, upande wa mashariki mwa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini mwa Lebona.
Yohana 4 : 5
5 ⑭ Basi akafika katika mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
Yohana 4 : 43
43 Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya.
Waamuzi 20 : 31
31 Nao wana wa Benyamini wakatoka waende kupigana nao, wakavutwa waende mbali na huo mji; kisha wakaanza kuwapiga na kuwaua Waisraeli wapatao thelathini, kama walivyofanya hapo awali, kwa kuwaua katika hizo njia kuu, zielekeazo Betheli, na Gibea, na katika nchi tambarare.
Kumbukumbu la Torati 19 : 3
3 Itengeze njia, igawanye na mipaka ya nchi yako, akurithishayo BWANA, Mungu wako, iwe mafungu matatu, ili kwamba kila mwenye kuua mtu apate kukimbilia huko.
Hesabu 20 : 17
17 tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kulia, wala upande wa kushoto, hadi tutakapotoka katika nchi yako.
Leave a Reply