Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Athalia
2 Wafalme 8 : 18
18 Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
2 Wafalme 8 : 26
26 ⑬ Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli.
2 Wafalme 11 : 3
3 ⑯ Alikuwako pamoja naye, amefichwa nyumbani mwa BWANA, miaka sita. Naye Athalia akaitawala nchi.
2 Wafalme 11 : 16
16 Basi wakampisha njia; akaenda kwa njia ya kuingia kwa farasi nyumbani mwa mfalme; akauawa huko.
2 Wafalme 11 : 20
20 Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia. Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme.
2 Mambo ya Nyakati 22 : 12
12 Akawako pamoja nao, amefichwa nyumbani mwa Mungu, miaka sita. Na Athalia akaitawala nchi.
2 Mambo ya Nyakati 23 : 15
15 Basi wakampisha njia; akaenda kwa kuingia pa mlango wa farasi nyumbani mwa mfalme; nao wakamwua huko.
2 Mambo ya Nyakati 23 : 21
21 ④ Basi wakafurahi watu wote wa nchi, na mji ukatulia baada ya Athalia kuuawa kwa upanga.
1 Mambo ya Nyakati 8 : 26
26 Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia;
Ezra 8 : 7
7 Na wa wana wa Elamu, Yeshaya, mwana wa Athalia; na pamoja naye wanaume sabini.
Leave a Reply