Biblia inasema nini kuhusu asubuhi – Mistari yote ya Biblia kuhusu asubuhi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia asubuhi

Zaburi 143 : 8
8 Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.

Zaburi 5 : 3
3 BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.

Yohana 1 : 1 – 51
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.
8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
15 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
16 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
19 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
20 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.
21 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
22 Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe?
23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.
25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?
26 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.
27 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya kiatu chake.
28 Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.
29 Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
31 Wala mimi sikumjua; lakini ili adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nilikuja nikibatiza kwa maji.
32 ① Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.
33 ② Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenituma kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.
34 ③ Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
35 Tena kesho yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.
36 ④ Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!
37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
39 Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
40 ⑤ Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
41 ⑥ Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
42 ⑦ Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
43 ⑧ Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.
44 Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro.
45 ⑩ Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.
46 ⑪ Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.
47 ⑫ Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.
49 ⑬ Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli.
50 Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya.
51 ⑭ Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Mithali 3 : 1 – 35
1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
3 ① Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
5 ③ Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 ④ Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
7 ⑤ Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
8 Itakuwa afya mwilini pako,[1] Na mafuta mifupani mwako.
9 ⑥ Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10 ⑦ Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na vyombo vyako vitafurika divai mpya.
11 ⑧ Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
12 ⑩ Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.
13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 ⑪ Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 ⑫ Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 ⑬ Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 ⑭ Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.
18 ⑮ Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye.
19 ⑯ Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
20 ⑰ Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande.
21 Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara.
22 Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako.
23 Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa.
24 ⑱ Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.
25 Usiogope hofu ya ghafla, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
26 Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
27 ⑲ Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
28 ⑳ Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe.
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
30 Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote.
31 Usimhusudu mtu mwenye ujeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
32 Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
33 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
34 Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.
35 Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *