Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Askari
Waamuzi 20 : 10
10 nasi tutatwaa watu kumi katika mia moja katika kabila zote za Israeli, na watu mia moja katika elfu, na watu elfu katika elfu kumi, ili waende kuwatwalia watu vyakula, ili hapo watakapofika Gibea ya Benyamini wapate kutenda mfano wa upumbavu huo wote walioutenda wao katika Israeli.
Nahumu 2 : 3
3 Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kukusanywa kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.
Kumbukumbu la Torati 20 : 8
8 Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.
Waamuzi 7 : 3
3 ③ Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu yeyote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu elfu ishirini na mbili wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.
Kumbukumbu la Torati 20 : 9
9 Itakuwa hapo watakapokwisha wale makamanda kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu.
Kumbukumbu la Torati 24 : 5
5 ④ Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.
Luka 3 : 14
14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Mathayo 27 : 31
31 ③ Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha.
Marko 15 : 20
20 Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakampeleka nje ili wamsulubishe.
Luka 23 : 11
11 Basi Herode akamdhalilisha, pamoja na askari wake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
Luka 23 : 37
37 huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe.
Luka 22 : 4
4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.
Mathayo 27 : 27
27 ① Ndipo askari wa mtawala wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio,[8] wakamkusanyikia kikosi kizima.
Mathayo 27 : 37
37 Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.
Marko 15 : 24
24 Wakamsulubisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini.
Yohana 19 : 24
24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.
Leave a Reply