Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia asili
Zaburi 145 : 5
5 Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.
Ayubu 12 : 7 – 10
7 Lakini sasa waulize hao wanyama, nao watakufundisha; Na ndege wa angani, nao watakuambia;
8 Au nena na nchi, nayo itakufundisha; Nao samaki wa baharini watakutangazia.
9 Katika hawa wote ni yupi asiyejua, Kwamba ni mkono wa BWANA uliofanya haya?
10 Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, Na pumzi zao wanadamu wote.
Mhubiri 3 : 11
11 ⑬ Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Isaya 55 : 12
12 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya shambani itapiga makofi.
Zaburi 69 : 34
34 Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake.
Warumi 8 : 19 – 22
19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;
21 kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina uchungu pamoja hata sasa.
Nehemia 9 : 6
6 Ezra akasema,[15] Wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako; wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vitu vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote; na jeshi la mbinguni lakusujudu wewe.
Zaburi 102 : 25
25 ② Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako.
Zaburi 23 : 1 – 6
1 BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Mathayo 6 : 28 – 30
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 ⑦ nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
Mwanzo 1 : 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Mwanzo 9 : 1
1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.
Leave a Reply