Biblia inasema nini kuhusu Ashtorethi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ashtorethi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ashtorethi

Yeremia 7 : 18
18 Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

Waamuzi 2 : 13
13 Wakamwacha BWANA, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.

Waamuzi 10 : 6
6 Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.

1 Samweli 7 : 4
4 Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia BWANA peke yake.

1 Samweli 12 : 10
10 Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa tuokoe kutoka kwa mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe.

1 Wafalme 11 : 5
5 ④ Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu wa kike wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

1 Wafalme 11 : 33
33 kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.

2 Wafalme 23 : 13
13 ⑱ Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kulia wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.

1 Samweli 31 : 10
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-sheani.

2 Wafalme 23 : 13
13 ⑱ Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kulia wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *