Biblia inasema nini kuhusu Ashtarothi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ashtarothi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ashtarothi

Kumbukumbu la Torati 1 : 4
4 alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei;

Yoshua 9 : 10
10 ⑭ na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng’ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.

Yoshua 12 : 4
4 tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,

Yoshua 13 : 31
31 ⑦ na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.

1 Mambo ya Nyakati 6 : 71
71 Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;

Mwanzo 14 : 5
5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *