Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ashkeloni
Yoshua 13 : 3
3 kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Waamuzi 1 : 18
18 Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.
Waamuzi 14 : 19
19 Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
1 Samweli 6 : 17
17 Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa BWANA; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja;
Yeremia 25 : 20
20 na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;
Yeremia 47 : 5
5 Upaa umeupata Gaza; Ashkeloni umenyamazishwa Mabaki ya bonde lao; Hata lini utajikatakata?
Yeremia 47 : 7
7 Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.
Amosi 1 : 8
8 Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
Sefania 2 : 4
4 Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang’olewa.
Sefania 2 : 7
7 Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watachunga makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajia na kuwarudisha wafungwa wao.
Zekaria 9 : 5
5 ⑩ Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana matarajio yake yatatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu.
Leave a Reply