Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Aramu
Hesabu 23 : 7
7 Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 23
23 ⑰ Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.
Mwanzo 10 : 23
23 Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 17
17 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
Mwanzo 22 : 21
21 Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu;
1 Mambo ya Nyakati 7 : 34
34 Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.
Leave a Reply