Biblia inasema nini kuhusu apocalypse – Mistari yote ya Biblia kuhusu apocalypse

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia apocalypse

Mathayo 24 : 36
36 ④ Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

Ufunuo 7 : 1 – 17
1 ⑲ Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai; akawaita kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,
3 ⑳ akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi tutakapokwisha kuwatia mhuri watumishi wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
4 Nikasikia hesabu yao waliotiwa mhuri katika kila kabila la Waisraeli, watu elfu mia moja na arubaini na nne.
5 Wa kabila la Yuda elfu kumi na mbili waliotiwa mhuri. Wa kabila la Reubeni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Gadi elfu kumi na mbili.
6 Wa kabila la Asheri elfu kumi na mbili. Wa kabila la Naftali elfu kumi na mbili. Wa kabila la Manase elfu kumi na mbili.
7 Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili.
8 Wa kabila la Zabuloni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Yusufu elfu kumi na mbili. Wa kabila la Benyamini elfu kumi na mbili waliotiwa mhuri.
9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-kondoo.
11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifudifudi mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala joto iliyo yote.
17 Kwa maana huyo Mwana-kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Yohana 3 : 1 – 33
1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
9 Nikodemo akajibu, akamwambia, Mambo haya yawezaje kuwa?
10 Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?
11 Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo tunalinena, na lile tuliloliona tunalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali.
12 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?
13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.
14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
20 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
22 Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka katika nchi ya Yudea; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.
23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.
24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani.
25 Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso.
26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.
27 ① Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.
28 ② Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nilisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.
29 ③ Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
30 ④ Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.
31 ⑤ Yeye ajaye kutoka juu, huyo yuko juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yuko juu ya yote.
32 ⑥ Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.
33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia mhuri ya kwamba Mungu ni kweli.

Ufunuo 17 : 8 – 10
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja itampasa kukaa muda mfupi.

Ufunuo 12 : 1 – 17
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, akiwa na uchungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto wa kiume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hadi kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika wake wakapigana na lile joka, lile joka nalo likapigana nao pamoja na malaika wake;
8 lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka lile lilipoona ya kuwa limetupwa katika nchi, lilimfuatia mwanamke yule aliyemzaa mtoto wa kiume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, ili achukuliwe na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule lililoutoa lile joka katika kinywa chake.
17 Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.

Wafilipi 2 : 14 – 17
14 ① Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,
15 ② mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
16 ③ mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.
17 ④ Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *