Biblia inasema nini kuhusu Amasa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Amasa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Amasa

2 Samweli 17 : 25
25 Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 17
17 ⑭ Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.

2 Samweli 17 : 25
25 Naye Absalomu akamweka Amasa awe juu ya jeshi mahali pa Yoabu. Basi huyo Amasa alikuwa mwana wa mtu, jina lake Yetheri, Mwishmaeli, aliyeingia kwa Abigali, binti Nahashi, nduguye Seruya, mamaye Yoabu.

2 Samweli 19 : 13
13 Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.

2 Samweli 20 : 12
12 Lakini Amasa alikuwa anagaagaa katika damu yake katikati ya njia kuu. Basi yule mtu alipowaona watu wote wamesimama, akamwondoa Amasa toka njia kuu akamtia kondeni, akamfunika nguo, hapo alipoona ya kuwa kila mtu aliyefika kwake amesimama.

1 Wafalme 2 : 5
5 ⑥ Na zaidi ya hayo, unajua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kumwaga damu wakati wa amani akilipiza kisasi cha vita, mshipi akautia damu ya vita uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.

1 Wafalme 2 : 32
32 Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 12
12 Ndipo wakaondoka juu ya hao waliotoka vitani baadhi ya wakuu wa wana wa Efraimu, Azaria, mwana wa Yohanani, na Berekia mwana wa Meshilemothi, na Yehizkia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *