Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Amaleki
Mwanzo 36 : 12
12 Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 36
36 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
Mwanzo 14 : 7
7 ⑱ Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Leave a Reply