Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Alexandria
Matendo 6 : 9
9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
Matendo 27 : 6
6 Na huko yule ofisa akakuta merikebu ya Aleksandria, tayari kusafiri kwenda Italia, akatupandisha humo.
Matendo 28 : 11
11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Aleksandria iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.
Matendo 18 : 24
24 Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, msemaji mzuri, akafika Efeso; naye alikuwa na ujuzi wa Maandiko.
Leave a Reply