Ahazia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ahazia

2 Mambo ya Nyakati 21 : 17
17 nao wakakwea juu ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asibakizwe mtoto hata mmoja, ila Ahazia,[22] aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe.

2 Mambo ya Nyakati 25 : 23
23 Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia,[29] huko Beth-shemeshi, akamchukua mpaka Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu, toka lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, dhiraa mia nne.

2 Wafalme 8 : 29
29 ⑮ Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli majeraha waliyotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.

2 Wafalme 9 : 29
29 Katika mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu, Ahazia alianza kutawala juu ya Yuda.

2 Wafalme 12 : 18
18 Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu.

2 Wafalme 10 : 14
14 Akasema, Wakamateni wa hai. Wakawakamata wa hai, wakawaua penye birika ya nyumba ya kukatia manyoya kondoo, watu arubaini na wawili; wala hakumsaza mtu wao awaye yote.

2 Mambo ya Nyakati 22 : 12
12 Akawako pamoja nao, amefichwa nyumbani mwa Mungu, miaka sita. Na Athalia akaitawala nchi.

1 Wafalme 22 : 40
40 Basi Ahabu akalala na baba zake; na Ahazia mwanawe akatawala mahali pake.

1 Wafalme 22 : 49
49 Ndipo Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, Watumishi wangu na waende pamoja na watumishi wako merikebuni. Lakini Yehoshafati hakukubali.

1 Wafalme 22 : 53
53 Akamtumikia Baali, akamwabudu, akamghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa mfano wa mambo yote aliyoyafanya baba yake.

2 Mambo ya Nyakati 20 : 37
37 ⑮ Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii juu ya Yehoshafati, akasema, Kwa sababu umepatana na Ahazia, BWANA amezivunjavunja kazi zako. Zikavunjika merikebu, zisiweze kufika Tarshishi.

2 Wafalme 3 : 1
1 Basi Yoramu[2] mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *