Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Adulamu
1 Samweli 22 : 1
1 Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko.
2 Samweli 23 : 13
13 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
1 Mambo ya Nyakati 11 : 15
15 ⑫ Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.
Zaburi 57 : 11
11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
Zaburi 142 : 7
7 Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.
Mwanzo 38 : 1
1 ⑳ Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
Yoshua 12 : 15
15 mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;
Yoshua 15 : 35
35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka;
2 Mambo ya Nyakati 11 : 7
7 Beth-suri, Soko, Adulamu,
Nehemia 11 : 30
30 Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakakaa toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
Mika 1 : 15
15 Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki; Utukufu wa Israeli utafika Adulamu.
Leave a Reply