Biblia inasema nini kuhusu Absalomu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Absalomu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Absalomu

2 Samweli 3 : 3
3 ⑫ na wa pili wake Danieli, wa Abigaili mkewe Nabali wa Karmeli; na wa tatu Absalomu, mwana wa Maaka binti Talmai, mfalme wa Geshuri,

1 Mambo ya Nyakati 3 : 2
2 wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;

2 Samweli 14 : 25
25 Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake.

2 Samweli 13 : 29
29 Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia.

2 Samweli 13 : 38
38 Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu.

2 Samweli 14 : 24
24 Naye mfalme akasema, Ageukie nyumbani kwake, asinione uso wangu. Basi Absalomu akarejea nyumbani kwake, asimwone uso mfalme.

2 Samweli 15 : 6
6 ⑩ Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli.

2 Samweli 15 : 13
13 ⑮ Mjumbe akamfikia Daudi, akasema, Mioyo ya watu wa Israeli inashikamana na Absalomu.

2 Samweli 18 : 17
17 Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake rundo kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.

2 Samweli 18 : 33
33 Naye mfalme akataabika sana, akapanda juu, akaingia kile chumba kilichokuwa juu ya lango, akalia; na katika kwenda kwake alisema hivi, Mwanangu Absalomu! Ee mwanangu! Mwanangu Absalomu! Laiti ningalikufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!

2 Samweli 19 : 8
8 Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.

2 Samweli 14 : 27
27 Kisha wakazaliwa kwake Absalomu wana watatu na binti mmoja, ambaye jina lake aliitwa Tamari; naye alikuwa mwanamke mzuri wa uso.

2 Samweli 18 : 18
18 Huyo Absalomu alipokuwa yu hai alikuwa ameitwaa na kujiinulia ile nguzo iliyoko bondeni mwa mfalme; kwa maana alisema, Mimi sina mtoto wa kuliendeleza jina langu; akaiita hiyo nguzo kwa jina lake mwenyewe nayo inaitwa mnara wa Absalomu hata hivi leo.

1 Wafalme 15 : 2
2 ③ Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu.

2 Mambo ya Nyakati 11 : 20
20 Kisha baada yake akamwoa Maaka, binti Absalomu; na yeye akamzalia Abiya, na Atai, na Ziza, na Shelomithi.

2 Samweli 18 : 18
18 Huyo Absalomu alipokuwa yu hai alikuwa ameitwaa na kujiinulia ile nguzo iliyoko bondeni mwa mfalme; kwa maana alisema, Mimi sina mtoto wa kuliendeleza jina langu; akaiita hiyo nguzo kwa jina lake mwenyewe nayo inaitwa mnara wa Absalomu hata hivi leo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *