Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Abiramu
Hesabu 26 : 10
10 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.
Kumbukumbu la Torati 11 : 6
6 ⑰ na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
Zaburi 106 : 17
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
1 Wafalme 16 : 34
34 Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Leave a Reply