Abinadabu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Abinadabu

1 Samweli 7 : 2
2 Ikawa, tangu sanduku lipelekwe Kiriath-yearimu, muda mrefu ulipita; maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Waisraeli wakamwombolezea BWANA.

2 Samweli 6 : 4
4 Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la BWANA; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku.

1 Mambo ya Nyakati 13 : 7
7 Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio wakaliendesha lile gari.

1 Samweli 16 : 8
8 Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, BWANA hakumchagua huyu.

1 Samweli 17 : 13
13 ① Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya, mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu Shama.

1 Samweli 14 : 49
49 ③ Basi, wana wa Sauli walikuwa ni hawa, Yonathani, na Ishvi, na Malkishua; na majina ya binti zake wawili yalikuwa haya; jina lake wa kwanza aliitwa Merabu, na jina lake mdogo aliitwa Mikali;

1 Samweli 31 : 2
2 Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli.

1 Wafalme 4 : 11
11 Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *