Abihu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Abihu

Kutoka 6 : 23
23 Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

Hesabu 3 : 2
2 ⑯ Tena majina ya hao wana wa Haruni ni haya; Nadabu mzaliwa wa kwanza, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

Kutoka 24 : 9
9 Ndipo akakwea juu, Musa, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli;

Kutoka 28 : 1
1 Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.

Mambo ya Walawi 10 : 2
2 Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na ukawateketeza, nao wakafa mbele za BWANA.

Hesabu 26 : 61
61 Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA.

Hesabu 3 : 4
4 ⑱ Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za BWANA, waliposongeza moto wa kigeni[3] mbele za BWANA, katika jangwa la Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani wakati wa uhai wa Haruni baba yao.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *