*# _DHAMBI ITAZUIA KUDHIHIRISHWA KWA BARAKA MWILINI._* *Maandiko ya Kiini* *1 Samweli 13:13-14* _”Ni upumbavu ulioje!” Samweli alishangaa. “Hukuishika amri aliyokupa Bwana, Mungu wako; kama ungeishika,_ *_BWANA angaliufanya ufalme wako juu ya Israeli kuwa imara milele._* *Ufahamu* Dhambi inaweza kuzuia udhihirisho wa kimwili wa baraka za Mungu kwa maisha yetu na leo tunaona mfano wa mfalme Sauli Nabii Samweli anamwambia mfalme Sauli kama hakutenda dhambi [kutotii amri za Mungu], ufalme wake utakuwa umeimarishwa milele, uzao baada ya uzao Sasa leo tofauti na wakati wa Sauli naamini mtu aliyezaliwa mara ya pili ameshabarikiwa *2Petro 1:3* na dhambi hiyo bado ni kikwazo kikubwa cha udhihirisho wa *_kimwili_* wa baraka za Mungu kwetu tulio ndani ya Kristo Yesu ni viumbe vipya *2Wakorintho 5;17*, tuliozaliwa kwa mbegu isiyoharibika *1Petro 1:23* roho ambazo haziwezi kutiwa unajisi na dhambi. Hata hivyo nafsi na mwili wetu vinaharibika, havijakombolewa na vinaweza kuzuia mtiririko wa baraka nyingi za Mungu kutoka kwa roho zetu. Basi tusiwe na mazoea ya kutenda dhambi *1 Yohana 3:9* kwani itatugharimu udhihirisho wa baraka za Mungu katika ulimwengu wa mwili. *OMBI* Bwana tunakushukuru kwa wingi wa mahitaji yetu yote katika roho. Utusaidie tusizuie udhihirisho wa baraka zako kwa kudumu katika dhambi. Amina
Leave a Reply