Biblia inasema nini kuhusu Zoari – Mistari yote ya Biblia kuhusu Zoari

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zoari

Mwanzo 13 : 10
10 ⑧ Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.

Kumbukumbu la Torati 34 : 3
3 na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari.

Isaya 15 : 5
5 Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.

Yeremia 48 : 34
34 ⑦ Toka kilio cha Heshboni mpaka Eleale, naam, mpaka Yahasa, wametoa sauti zao, toka Soari mpaka Horonaimu, hata Eglath-shelishia; maana maji ya Nimrimu nayo yatakuwa ukiwa.

Mwanzo 14 : 2
2 ⑯ walifanya vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari.

Mwanzo 14 : 8
8 Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu;

Mwanzo 19 : 23
23 Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari.

Mwanzo 19 : 30
30 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *