Biblia inasema nini kuhusu Zipor – Mistari yote ya Biblia kuhusu Zipor

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zipor

Hesabu 22 : 2
2 ⑰ Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori.

Hesabu 22 : 4
4 ⑲ Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng’ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.

Hesabu 22 : 10
10 Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema,

Hesabu 22 : 16
16 Wakamfikia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lolote lisikuzuie usinijie;

Hesabu 23 : 18
18 ⑤ Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;

Yoshua 24 : 9
9 ⑦ Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu kumwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *