Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zawadi
Kutoka 20 : 6
6 ⑱ nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kutoka 20 : 12
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Waefeso 6 : 3
3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
Mambo ya Walawi 25 : 19
19 Nayo nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuishi humo salama.
Mambo ya Walawi 26 : 45
45 ⑯ lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi BWANA.
Kumbukumbu la Torati 4 : 40
40 Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.
Kumbukumbu la Torati 6 : 3
3 Sikiliza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali.
Kumbukumbu la Torati 6 : 18
18 Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako,
Kumbukumbu la Torati 11 : 16
16 Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu;
Kumbukumbu la Torati 11 : 21
21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Kumbukumbu la Torati 11 : 29
29 Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali.
Kumbukumbu la Torati 27 : 26
26 ⑲ Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Yoshua 8 : 33
33 ② Na Israeli wote pamoja na wazee, viongozi wao na waamuzi wao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyoamuru hapo awali, ili wawabariki watu wa Israeli.
Kumbukumbu la Torati 15 : 11
11 ⑥ Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
Kumbukumbu la Torati 22 : 7
7 ⑲ sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi.
Kumbukumbu la Torati 24 : 19
19 ⑯ Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
Kumbukumbu la Torati 25 : 15
15 Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Isaya 1 : 20
20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.
Isaya 3 : 10
10 Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
Isaya 40 : 11
11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Yeremia 22 : 4
4 ⑯ Kwa maana mkifanya haya kweli kweli, ndipo watakapoingia kwa malango ya nyumba hii wafalme wenye kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi, wanakwenda kwa magari, na wamepanda farasi, yeye, na watumishi wake, na watu wake.
Yeremia 17 : 26
26 ⑥ Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela,[2] na milima, na upande wa Negebu,[3] wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA
Mathayo 10 : 32
32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Luka 12 : 8
8 Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Mtu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;
Mathayo 16 : 27
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mathayo 20 : 16
16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.
Mathayo 25 : 46
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Marko 10 : 21
21 ⑯ Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Leave a Reply