Biblia inasema nini kuhusu Zakaria – Mistari yote ya Biblia kuhusu Zakaria

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Zakaria

2 Wafalme 10 : 30
30 ⑪ BWANA akamwambia Yehu, Kwa kuwa umetenda vema kwa kufanya vilivyo haki machoni pangu, kuitendea nyumba ya Ahabu sawasawa na yote yaliyomo moyoni mwangu, wana wako wa kizazi cha nne watakaa kitini mwa Israeli.

2 Wafalme 14 : 29
29 Yeroboamu akalala na babaze, yaani, na wafalme wa Israeli. Na Zekaria mwanawe akatawala mahali pake.

2 Wafalme 15 : 12
12 Hilo ndilo neno la BWANA alilomwambia Yehu, akisema, Wana wako watakaa kitini mwa Israeli hata kizazi cha nne. Ikawa vivyo hivyo.

2 Wafalme 18 : 2
2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.

2 Mambo ya Nyakati 29 : 1
1 Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na tisa; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *