Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia zaka
Malaki 3 : 8 – 10
8 ② Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 ③ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
2 Wakorintho 9 : 6 – 8
6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Malaki 3 : 8
8 ② Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
Mambo ya Walawi 27 : 30
30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.
Mithali 3 : 9
9 ⑥ Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Mathayo 23 : 23
23 ⑯ Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
Hagai 2 : 8
8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi.
Waraka kwa Waebrania 7 : 1 – 28
1 ② Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
2 ambaye Abrahamu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
3 ③ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
4 Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.
5 ④ Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika uzao wa Abrahamu.
6 Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Abrahamu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.
7 Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.
8 Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yuko hai.
9 Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Abrahamu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;
10 kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.
11 Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine awepo, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?
12 Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.
13 Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hilo aliyeihudumia madhabahu.
14 ⑤ Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani.
15 Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kama Melkizedeki;
16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo;
17 ⑥ maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
18 Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;
19 ⑦ (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo tunamkaribia Mungu.
20 Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,
21 ⑧ (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;)
22 ⑩ basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae;
24 bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
25 ⑪ Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
26 ⑫ Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
27 ⑬ ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.
28 ⑭ Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Kumbukumbu la Torati 14 : 28 – 29
28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la mavuno yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;
29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Mathayo 6 : 1 – 4
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Luka 6 : 38
38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Kumbukumbu la Torati 14 : 22 – 26
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
23 Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima.
24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako;
25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako;
26 na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Matendo 20 : 35
35 Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
Mwanzo 28 : 20 – 22
20 ⑮ Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
21 ⑯ nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.
22 ⑰ Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Luka 11 : 42
42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.
Marko 12 : 41 – 44
41 ⑱ Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.⑲
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
44 ⑳ maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Warumi 13 : 7
7 ② Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Malaki 3 : 6 – 10
6 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
7 ① Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
8 ② Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 ③ Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Mwanzo 28 : 22
22 ⑰ Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Mambo ya Walawi 27 : 1 – 360
1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 ⑱ Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa BWANA, kama utakavyowahesabia wewe.
3 ⑲ Na hesabu yako itakuwa kwa mwanamume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.
4 Kama ni mwanamke, hesabu yako itakuwa shekeli thelathini.
5 Tena akiwa na umri wa miaka mitano hata umri wa miaka ishirini, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli ishirini kwa mwanamume, na shekeli kumi kwa mwanamke.
6 Tena akiwa na umri wa mwezi mmoja hadi miaka mitano, ndipo hesabu yako itakuwa shekeli tano za fedha kwa mwanamume na shekeli tatu za fedha kwa mwanamke.
7 Tena akiwa na umri wa miaka sitini na kuzidi; kama ni mwanamume, hesabu yako itakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke shekeli kumi.
8 ⑳ Lakini akiwa ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamkadiria; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomkadiria.
9 Tena kama ni mnyama wa namna ambayo watu husongeza kuwa sadaka kwa BWANA, kila mmoja katika wanyama hao atakayetolewa kwa BWANA, na mtu yeyote, atakuwa ni mtakatifu.
10 Yeye hatamgeuza, wala kumbadili mwema kwa mbaya, au mbaya kwa mwema; ikiwa atabadili mnyama kwa mnyama yeyote, ndipo mnyama huyo na yule waliobadiliwa wote wawili watakuwa watakatifu.
11 Na kama ni mnyama yeyote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa BWANA, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani;
12 na kuhani atamkadiria, akiwa mwema akiwa mbaya; kama kuhani atakavyomkadiria, ndivyo itakavyokuwa.
13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.
14 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa BWANA ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa.
15 Tena mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali yake.
16 Tena kama mtu akiweka wakfu kwa BWANA sehemu ya shamba la milki yake, ndipo hesabu yako itakuwa kama kule kupanda kwake kulivyo; kupanda kwake homeri moja ya mbegu ya shayiri, kutahesabiwa kuwa ni shekeli hamsini za fedha.
17 Ikiwa anaweka shamba lake liwe wakfu tangu mwaka wa jubilii, litakadiriwa vivyo hivyo kama hesabu yako ilivyo.
18 Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya jubilii, ndipo kuhani atamhesabia hiyo fedha kama hesabu ya miaka iliyobaki hata mwaka wa jubilii, na kuhesabiwa kwako kutapunguzwa.
19 Na kama yeye aliyeliweka shamba wakfu akitaka kulikomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nalo litathibitishwa kwake.
20 Lakini asipotaka kulikomboa shamba, au kama amemwuzia mtu mwingine hilo shamba, halitakombolewa tena kabisa;
21 ila hilo shamba litakuwa takatifu kwa BWANA litakapotoka katika jubilii, kama ni shamba lililowekwa wakfu; litakuwa mali ya kuhani.
22 Tena kama akiweka wakfu kwa BWANA shamba ambalo amelinunua, ambalo si shamba la milki yake;
23 ndipo kuhani atamhesabia kima cha kuhesabu kwako hata mwaka wa jubilii: naye atatoa siku hiyo kama hesabu yako, kuwa ni kitu kitakatifu kwa BWANA.
24 Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake.
25 Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja.
26 Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa BWANA, mtu yeyote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng’ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa BWANA.
27 Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo.
28 Pamoja na hayo, hakitauzwa wala kukombolewa kitu chochote kilichowekwa wakfu, ambacho mtu amekiweka wakfu kwa BWANA, katika vitu vyote alivyo navyo, kama ni mtu, au mnyama, au kama ni shamba la milki yake; kila kitu kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa BWANA.
29 Kila aliyewekwa wakfu, aliyewekwa wakfu na binadamu, hatakombolewa; sharti atauawa.
30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.
31 Na kama mtu akitaka kukomboa chochote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.
32 Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA.
33 Hataangalia kama ni mwema au ni mbaya, wala hatambadili; na kama akimbadili na yoyote, ndipo wote wawili, huyo na huyo waliobadiliwa watakuwa ni watakatifu; hatakombolewa.
34 Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.
Leave a Reply