Biblia inasema nini kuhusu zaburi – Mistari yote ya Biblia kuhusu zaburi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia zaburi

Isaya 40 : 8
8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Zaburi 91 : 1 – 16
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji, Na katika maradhi mabaya.
4 ⑳ Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hatari za usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala mapigo yajayo usiku, Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7 Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako. Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia! Wewe hutakaribiwa na maafa.
8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonesha wokovu wangu.

Zaburi 23 : 1 – 6
1 BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Zaburi 27 : 1 – 14
1 BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
2 Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
3 Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumainia BWANA.
4 Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.
5 Maana atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
6 Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
7 Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia, Unifadhili, unijibu.
8 Uliposema, “Nitafuteni uso wangu,” Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.
9 Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
10 Hata baba yangu na mama yangu wakiniacha, Bali BWANA atanikaribisha kwake.
11 Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
12 Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.
13 ① Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.
14 ② Umtumainie BWANA, uwe imara, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Zaburi 37 : 1 – 40
1 Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2 Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.
3 Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.
5 Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumainie, naye atakutendea.
6 Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9 Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
10 Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
11 Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
12 Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.
13 BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
14 Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, Wamwangushe chini maskini na mhitaji, Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15 Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe, Na nyuta zao zitavunjika.
16 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17 Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18 BWANA huwatunza waaminifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22 Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi, Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali.
23 Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake.
24 Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.
27 Jiepushe na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele.
28 Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
30 Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu.
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.
32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumwua.
33 BWANA hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamwacha alaumiwe atakapohukumiwa.
34 Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
35 Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
36 Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana.
37 Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
38 Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.
39 Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
40 Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *