Biblia inasema nini kuhusu Yosia – Mistari yote ya Biblia kuhusu Yosia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Yosia

2 Wafalme 21 : 26
26 Akazikwa kaburini mwake katika bustani ya Uza. Na Yosia mwanawe akatawala mahali pake.

2 Wafalme 22 : 1
1 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi.

1 Mambo ya Nyakati 3 : 14
14 na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.

2 Mambo ya Nyakati 33 : 25
25 Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfanyia fitina mfalme Amoni; watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme badala yake.

Mathayo 1 : 11
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

2 Wafalme 23 : 30
30 Watumishi wake wakamchukua garini, amekwisha kufa, kutoka Megido, wakamleta Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake mwenyewe. Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, wakamtawaza awe mfalme badala ya baba yake.

2 Mambo ya Nyakati 35 : 24
24 Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakamlilia Yosia.

2 Mambo ya Nyakati 35 : 25
25 Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.

2 Wafalme 22 : 7
7 Lakini hawakuulizwa habari za ile fedha waliyokabidhiwa; maana walitenda kazi kwa uaminifu.

2 Mambo ya Nyakati 34 : 4
4 ④ Wakazibomoa madhabahu za mabaali machoni pake; na sanamu za jua, zilizoinuliwa juu yake, akazikatakata; Maashera, sanamu za kuchonga, na za kusubu, akazivunjavunja, akaziponda kuwa mavumbi, akayamimina juu ya makaburi ya hao waliozichinjia dhabihu.

2 Wafalme 22 : 20
20 ④ Kwa hiyo tazama, nitakukusanya pamoja na baba zako, nawe utawekwa kaburini mwako kwa amani; wala macho yako hayatauona uovu huo wote nitakaouleta juu ya mahali hapa. Basi wakamletea mfalme habari tena.

2 Mambo ya Nyakati 34 : 33
33 Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.

2 Wafalme 23 : 23
23 Bali katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia ilifanyika Pasaka hii kwa BWANA ndani ya Yerusalemu.

2 Mambo ya Nyakati 35 : 19
19 Katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Yosia ikafanyika Pasaka hiyo.

Mathayo 1 : 11
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

1 Wafalme 13 : 3
3 ⑪ Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena BWANA, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *